Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi kikombe Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma Salum Ally,
baada ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa kuwa mshindi wa jumla katika
maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8,
2012, wakati alipokuwa akifunga maonyesho hayo katika Viwanja vya
Nzuguni mjini Dodoma.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wajasiliamali wa vikundi vya wakulima,
wakati alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima
Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni
mjini Dodoma.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili wakati
walipowasili kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo Agosti 8, 2012
kwa ajili ya kufunga rasmi maonyesho hayo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete, kufunga
rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo
Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyesha Tuzo aliyokabidhiwa kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ikiwa
ni sehemu ya kutambua mchango wa Rais katika kusimamia na kuendeleza
Kilimo Kwanza, wakati Makamu alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya
Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma
leo Agosti 8, 2012. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Christopher Chiza.