Mgeni rasmi mkuu wa Wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba akisoma risala mbele ya makarani wa sensa waliofuzu mafunzo yao.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bi Theresia Mahongo akisisitiza jambi kabla ya kumkaribiasha mgeni Rasmi.
Makarani wa sensa wakimsikiliza mgeni rasmi.
Zaidi
ya Makarani 260 watakaoshiriki zoezi la sensa ya watu na makazi
Manispaa ya Iringa mjini wametakiwa kutenda kazi hiyo kwa moyo na
uaminifu mkubwa kama mafunzo yanavyosema ili taarifa zinazohitajika na
serikali kupitia zoezi hilo la sensa ziweze kufanikiwa.
Akizungumza
wakati wa kufunga mafunzo ya makarani wa sensa yaliyoendeshwa kwa muda
wa wiki moja Katika Manispaa ya Iringa Mjini, Mkuu wa Wilaya hiyo
Dkt. Leticia Warioba amesema anaamini makarani hao walipatiwa mafunzo
yao ipasavyo kama wakufunzi walivyowafundisha mafunzo hayo na kusema
wao wanategemewa kwa kiasi kikubwa kufanikisha zoezi hilo ambapo
serikali imedhamiria kukusanya takwimu ya watu na makazi ifikapo tarehe
26 August ikiwa ni moja ya vipaumbele vya taifa.
Ameongeza
kuwa madhumuni makubwa ya mafunzo hayo yalikuwa ni kuwawezesha na
makarani na wadadisi ili waweze kukusanya takwimu sahihi. Amesema endapo
watakiuka mafunzo waliyopatiwa kutapelekea zoezi hilo kutofanikiwa
hali ambayo haitegemewi na yeye pamoja na serikali kwa ujumla hivyo
wanatakiwa kutambua dhamana waliyokabidhiwa ni kubwa hivyo ni azima
waifanye kama inavyotakiwa.
Pia
amewataka kupambana na changamoto zitakazojitokeza na kuhakikisha
wanatoa taarifa mapema kwa wasimamizi wao mara moja pindi wanapokutana
na changamoto ili ziweze kutatuliwa haraka na zoezi la sensa liendelee.
Amewataka
viongozi wa dini, siasa na wananchi kutoa ushirikiano katika
kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hili la sensa.
Nakuwaomba wananchi kutunza kumbukumbu zote za taarifa za maswali
yatakayoulizwa kwa wale watu waliolala katika kaya zao usiku wa kuamkia
tarehe 26 Augusti mwaka huu. Nakuwataka wale ambao wana wake wengi kwa
maana ya mkuu wa kaya kutoa taarifa sahihi ili kufanikisha zoezi.
Picha kwa hisani ya http://francisgodwin.blogspot.com