Kiwango cha fedha cha msanii huyo ineosha kuwa anajua thamani yake kama msanii mkubwa anayehitaji kuwa lulu ndani ya tasnia hiyo. Baadhi ya filamu alizowahi kung’arisha mwanadada huyu ni pamoja na ‘Because of You’, ‘Love Me Or Love Me Not’ na nyingine nyingi.
Ndauka katika pozi
Akiongea na mwandishi wa mtandao wa DarTalk aliyetaka kujua kama Rose anatambua thamani yake, ambapo alidai kuwa kwa upande wake haoni sababu ya kuficha na kuendelea kuumia, na ndiyo maana ameamua kuweka wazi ishu hiyo kuwa hachezi filamu ya mtu bila muafaka wa kiwango cha fedha alichokitaja.
“Inatakiwa tufikie kipindi wasanii tujue thamani yetu kwani wapo baadhi ya wasanii wengine wana majina makubwa lakini wanafanya filamu kwa bei za chini, lakini siwezi kulaumu kwani kila mtu anafanya kwa mipango yake,” alidai.