Matukio Sikukuu ya Idd el Fitr
Bondia Maneno Oswald akitangazwa baada ya kumdunda Rashid Matumla.
Matumla akisulubiwa jukwaani wakati wa mpambano huo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Juma Kassim ‘Juma Nature’, akionyesha ukongwe wake.
Kiongozi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki zake.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Estelinah Sanga ‘Linah’, akiwa jukwaani.
Mwasiti Almasi akikamua na wacheza shoo wake.
Maunda Zorro akionyesha umaarufu wake.
Sadick Momba (kushoto), akipambana na Venance Mponji katika mpambano wa utangulizi ambapo Sadick aliibuka mshindi.
Julius Thomas (kushoto), akizidunda na Jumanne Kirumbe kabla ya Maneno
Oswald na Matumla kupanda ulingoni. Julius alishinda mpambano huo.
Mmoja wa wasanii wa kundi la Mabaga Fresh ambaye sasa yuko katika kundi la Wanaume Halisi, JB Mkuu wa Maadui akiwajibika.
Mwimbaji wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Khadija Yusuf akitumbiza jukwaani.
Malkia wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Leila Rashid akiwajibika.
Watoto wakicheza muziki ndani ya bwawa la kuogelea.
Baadhi ya umati uliokuwa ndani ya ukumbi huo.
MPAMBANO wa ndondi baina ya mabondia Maneno Oswald na Rashid Matumla
ambao ulifanyika ukumbi wa maraha wa Dar Live Mbagala, jijini Dar es
Salaam, katika kuadhimisha sikukuu ya Idd el Fitr, ulishuhudia Oswald
akimchakaza Matumla kwa pointi.
Mbali na mpambano huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo, kulikuwa pia na
burudani za aina mbalimbali, likiwemo disko la watoto ambao pia
walifurahia kuogelea katika bwawa maalum na michezo mingine mingi. Kwa
upande wa muziki kulikuwa na shoo kali zilizofanywa na wanamuziki Juma
Nature, Mwasiti Almasi, Estelinah Sanga ‘Linah’, Maunda Zorro na kundi
zima la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na mfalme, Mzee Yusuf.