Skyner alisema kuwa kutofanya kwake filamu kumetokana na kauli ya baba wa mtoto, hivyo hata kwa upande ameona ni bora asitishe ili aweze kumlea vizuri mwanaye, kwani bado ni mdogo na hataki kuwa naye mbali.
Alisema akiendelea kufanya filamu kwa kipindi hiki anaweza kumfanya mtoto wake alelewe na mfanyakazi kitu ambacho hataki, hivyo atakapotimiza umri mkubwa kidogo ataendelea na kazi ya filamu.
“Kwa sasa siwezi kufanya vizuri hadi pale mtoto wangu atakapotimiza miaka miwili na kuendelea, kwani nikiamua kurudi kwenye game naweza kuwa mbali na mtoto halafu inakuwa siyo vizuri kwani bado ni mdogo sana na kama unavyojua unaweza kuwa kambini kwa wiki mzima sasa utakuwa unakaa na mtoto kambini itakuwa siyo poa,” alisema.