“SITAKI KUOLEWA NA MTANZANIA” – WEMA SEPETU…!!

MSANII gumzo wa tasnia ya filamu bongo na miss tanzania pekee mwenye nyota kali ya kupendwa kuliko maelezo, Wema Sepetu, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa hawezi kuolewa Tanzania kwani hata akiamua kuchukua maamuzi hayo bado kuna watu wanaweza kumuharibia ndoa yake kwa sababu zao binafsi.
Msanii huyo alidai kuwa hawezi kuacha kuzungumza ukweli kwani watu hawapendi maisha yake na ndiyo maana kila siku hawaishiwi cha kusema juu yake na hata mahusiano yake ya kimapenzi.

Alidai kuwa kutokana na kuandamwa na skendo kadhaa wanaume wengi wanamini yeye ni mwanamke muhuni, na ndiyo maana hakuna anayetaka kumchumbia, hivyo anaamini hawezi kuvishwa pete na mwanaume wa kitanzania kwani tayari wameshalishwa maneno machafu juu yake.


“Unajua wapo watu ambao kazi yao ni kunichafua na hawapendi maendeleo yangu, na kwangu mimi naamini hata kama nikisema nataka kuolewa kuna watu watafanya juu na chini ili tu ndoa yangu isifungwe, hivyo naweza kufunga ndoa na mwanaume wa nchi za nje kwani hata mi mwenyewe sitaki wabongo,”
alidai.

Mwandishi wa
DarTalk, alipotaka kujua mahusiano yake na Diamond mwisho wake utakuwa vipi, alijibu  “Suala la mimi na Diamond halihusiani na ishu yangu ya kufunga ndoa na mwanaume wa nje kwani najua Diamond hawezi kuishi na mimi kwa sababu tayari naye anaanza kulishwa maneno kuwa anatembea na mwanamke mkubwa wakati miaka yangu ni midogo sana,” alidai.

Hata hivyo mtandao huo ulipotaka kujua kauli ya
Diamond juu ya Wema anaposema kuwa hawezi kuolewa na mwanaume wa kibongo, hivyo kwa upande wake anazungumziaje, lakini simu yake haikuweza kupokelewa baada ya kuita kwa muda mrefu.