Viwanjani Leo Jumatatu

Wachezaji wa Simba B wakiwa na kombe la ubingwa wa BankABC Super 8 baada ya kuichapa Mtibwa Sugar 4-3

Habari ya Eid ndugu zangu natumaini sikukuu imeenda vyema kwa Uweza wa Mungu , na nimatuamini yangu tumesherekea vizuri, 
siku ya leo sina neno refu zaidi ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya simba (Timu ya vijana) kwa kuonyesha soka safi katika mashindano ambayo yalishilikisha timu za wakubwa katika mashindano ya BankABC Super 8,

 Hii ni changamoto kwetu kwa vilabu vingine kuandaa timu za vijana naamini hapa wadau mtaungana nami katika wazo lango la kuandaa timu za vijana kuanzia mashuleni ipo haja ya kuanzisha shule nyingi za michezo hata ikibidi ziwe kila mkoa na zisimamiwe na wizara yenye dhamana katika kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, 

Hakika tukiweza kufanya zoezi ili hata ikibidi kwenye shule za kata tukaweka mtaala wa michezo hii itasaidia sana,  Tutafakari na huu ni wakati wa kuchukua hatua kwa maendeleo ya mchezo wa soka katika nchi yetu.  Sikukuu njema