UEFA CHAMPIONS LEAGUE: VIWANJA NANE KUWAKA MOTO ULAYA LEO.
MENEJA wa klabu ya
Manchester City, Roberto Mancini ametamba kuwa kikosi chake kimejiandaa
vyema kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Klabu Bingwa ya
Ulaya dhidi ya Real Madrid katika Uwanja wa Santiago Bernabeu baadae
usiku. Mancini
alitamba kuwa msimu huu amekiandaa kikosi chake vyema kwa ajili ya
kuhakikisha wanafika mbali kwenye michuano hiyo na watadhihirisha hilo
wakati watakapokutana na Madrid usiku wa leo. Mbali na mchezo huo pia
kutakuwa na michezo mingine ambapo Arsenal watakuwa wageni wa timu ya
Montpellier ya Ufaransa, AC Milan itaikaribisha Anderlech, Paris St
Germain-PSV itawakaribisha Dynamo Kiev huku mabingwa wa soka wa
Ujerumani Borussia Dortmund wataikaribisha Ajax Amsterdam. Michezo
mingine Malaga ya Hispania itaikaribisha Zenit St Petersburg ya Urusi,
Dinamo Zagreb itakuwa wenyeji wa FC Porto ya Ureno wakati Olympiacos ya
Uturuki itawakaribisha Schalke 04 ya Ujerumani.