|
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Usambazaji ya MY CollectionMUSSA MSUBA akiwa katika duka la mauzo ya kazi za Jahazi
|
MSANII
WA MZIKI WA TAARABU,MZEE YUSUFU KUSHOTO AKIANGALIA MOJA YA KAZI YAKE
ILIYOKUWA FEKI ZILIZOKAMATWA NA WASANII WENYEWE KWA KUSHIRIKIANA NA
KAMPUNI YA STEPS ENTANTAINMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM
MSANII wa mziki
wa Taarabu nchini Mzee Yussuf ameamua kufungua kampuni yake ya
usambazaji ijulikanayo kama MY Collection kwa ajili ya kusambaza kazi
zake
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Mussa Msuba
amesema wameamua kufungua duka kwa ajili ya kuuza CD NA DVD za bendi ya
Jahazi inayongozwa na Mzee Yussuf duka hilo lililopo makutano ya
barabara ya likoma na Muhonda
linalojihusisha
na huzwaji wa DVD za taarabu kwa jumla na rejareja kwa ajili ya
kuwaweka karibu wapenzi wake ili waweze kupata burudani kupitia nyimbo
zao kwa kuwaburudisha wakiwa majumbani
Msuba amesema
kuwa Mzee yusufu yupo mbioni kutoa albamu yake ya mduara itakayokuwa
hivi karibuni ambayo ni yake binafsi mbali na hilo bendi hiyo itatoa
video yake ya Live za albamu zake zote za Two in One,Kazi ya Mungu,
Nakula ka Naksh Naksh,tupendane,Daktari wa Mapenzi
Ambazo zitakuwa madukani kwa ajili ya kuwapa wapenzi wao burudani wakiwa majumbani mwao
Nae Mzee Yussuf
aliongeza kwa kusema ameanzisha Kampuni yake binafsi baada ya kuona
kwamba kazi zake nyingi zimekuwa zikichakachuliwa kutokana na kuwepo
kwa wizi wa kazi za Sanaa
Kampuni yake imekuwa ikisambaza kazi zake kwa ajili ya kuogopa kuibiwa kutokana na wimbi wa kazi za wasanii nchini
Duka lililopo
mtaa wa Muhonda na Likoma kwa ajili ya CD za Jahazi pekee mbali na
duka hilo mzee Yusufu anamiliki Duka lingine la Nguo lililopo Magomeni
Mapipa kwa ajili ya kujiongezea kipato chake mbali na bendi yake
Bendi ya Jahazi
mpaka sasa imekwisha toa albam nane ambazo zipo madukani zinauzwa kwa
ajili ya watu wotekupata burudani wakiwa majumbani mwao
Kwa sasa bendi
hiyo ipo mbioni kuachia albamu yake ya tisa ambayo aijapewa jina
inatarajiwa kuzinduliwa mwezo October kwa ajili ya kutoa burudani kwa
wapenzi wao na kuwataka mashabiki wao kuja kuangalia na kusikiliza
nyimbo mpya popote pale wanapotoa burudani zao katika kumbi mbalimbali
za jijini Dar es salaam
|
DUKA LA MZEE YUSSUF LILILOPO KATIKA MAKUTANO YA MTAA YA LIKOMA NA MUHONDA LINALOSAMBAZA KAZI ZA BENDI YA JAHAZI |