MADRID YAMCHUKUA ESSIEN KWA MKOPO.
KLABU ya Real Madrid ya
Hispania imetangaza kufikia makubaliano ya kumnyakuwa kiungo wa Chelsea
Michael Essien kwa mkopo katika kipindi chote cha msimu huu. Essien
mwenye miaka ambaye alijiunga na Chelsea mwaka 2005 akitokea klabu ya
Olympique Lyon ya Ufaransa anatua Madrid na kukutana na Jose mourinho
ambaye amewahi pia kuinoa klabu hiyo ya Uingereza. Mchezaji huyop
anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji akiwa na Chelsea amefanikiwa
kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu nchini humo, mataji manne ya Kombe la
FA na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Essien hakuwemo katika kikosi cha
Chelsea ambacho kilichabangwa mabao 4-1 na Atletico Madrid katika
mchezo wa Super Cup uliochezwa jijini Monaco, Ufaransa jana usiku.