BAADA ya msanii Irene Uwoya kudai kuwa msanii mwenzake Jackline Wolper
hana kiwango cha kuweza kushiriki naye kwenye filamu moja, naye Wolper
amejibu mapigo kuwa hata yeye haitaji kucheza naye kwani anaamini
kiwango chake si cha mdomoni bali mara zote anakionesha akiwa kazini na
hata mashabiki zake wanajua hilo.
Mtandao huu ulitumia nguvu ya ziada kutafuta Wolper
ambaye mara kadhaa simu yake ilikuwa imezimwa na baada kupatikana
msanii huyo alidai yuko bize ambapo aliamua kumtumia rafiki yake wa
karibu ili kujibu hoja, ambapo alidai kuwa hawezi kuzungumza chochote
kwani wanaosema yeye hana kiwango hawamjui na wanamuona juu juu
lakini hawajawahi kushiriki naye kwenye kazi ambayo inaweza kutoa majibu
yote.
Rafiki
huyo ambaye hata hivyo alikataa kujitambulisha jina, alidai
alichoambiwa akijibu ndicho anachokitoa, ambapo aliongeza kuwa kauli ya Uwoya haimshtui na ataendelea kusimama imara katika kila kazi anayotoa kwa lengo kuwapa ujumbe mashabiki wke.
“Kwangu
siwezi kujibu kauli za mtu ambaye hana uwelewa wa nini anachikisema
.Wanaoweza kutoa kauli kama hizo ni mashabiki na wapenzi wa kazi zetu,
hivyo nawaomba wadau wa wangu wasimsikilize mtu ambaye anakaribia
kupotea kwenye tasnia,”.
Hata hivyo baada ya kuachana na rafiki huyo mwandishi wa habari alizungumza tena na Wolper. ishu iliyobuka upya ni kwamba baada ya kudaiwa kuwa wameachana na mpenzi wake Dallas
na amepokonywa mkoko wenye thamani ya sh 175 m, Jack alikana habari
hizo na kudai kuwa yeye mwenyewe hajatamkiwa kuwa ameachwa.
“Hizo
habari hazina ukweli si unajua watu wakiamua kutoa ishu za uongo
wanatoa ili tu mtu aonekana mbaya, lakini najua nafasi yangu ni ipi ” alidai Wolper.