Prezzo & Goldie |
Aliyekuwa mmoja wa washiriki na wawakilishi wa Nigeria katika jumba la Big brother Stargame 2012 Goldie, jumamosi iliyopita 15thsept 2012 aliland katika ardhi ya Kibaki mishale ya midnight.
Kwa
mujibu wa mtandao mmoja wa Kenya Goldie alipokelewa uwanja wa ndege na
yule yule wanaepatana na kukosana mara kwa mara Prezzo, kitu
kinachowafanya watu wengi waamini kuwa sasa uhusiano kati ya Prezzo na
Goldie umerejea katika hali nzuri.
pamoja na Prezzo alikuwepo pia former house mate mwingine wa Big Brother aitwae Millicent Mugadi.
Muda
mfupi baada ya Goldie kuwasili uwanja wa ndege, mabegi yake
yalipelekwa katika Mercedez Benz E-Class rangi ya silver ya Prezzo
ambayo ndio iliyompeleka katika hotel aliyofikia.
Ujio
wa Goldie nchini Kenya umekuwa wa kimya kimya kitu kinachoashiria kuwa
yeye pamoja na mwenyeji wake Prezzo hawakupenda attention ya media.
Kwa
mujibu wa watu wa karibu, Goldie amesema atakuwepo Kenya kwa muda wa
wiki nzima au na zaidi, na lengo la safari yake hiyo ni kufanya
recording ya nyimbo, na kati ya nyimbo atakazo record anategemea
kumshrikisha Prezzo.
Ni
mwezi mmoja tu umepita toka Prezzo aende nchini Nigeria anakotoka
Goldie, kwa lengo la kukutana na Goldie ambaye mara yao ya mwisho kuwa
pamoja ilikuwa ni katika jumba la Big Brother ambapo Goldie alikuwa
evicted na kumwacha prezzo.