Meneja
wa muda mrefu wa 50 Cent, Diddy, Ja Rule, na Mariah Carey, Chris
Lighty amepatikana akiwa amekufa jana asubuhi jijini New York katika
kile kinachoonekana kama kajiua kwa kujipiga risasi.
Kwa
mujibu wa polisi, mwili wa meneja huyo aliyekuwa na miaka 44
ulipatikana saa 11:30 AM kwa saa za Marekani kwenye nyumba yake ya
Bronx. Kifo hicho kinachunguzwa kama kitemetokana na kujiua mwenyewe.
Kwa mujibu wa vyanzo, Lighty, alikuwa na majibizano na mke wake wa zamani na kuamua kujipiga risasi kichwani.
Yeye na mke wake walipeana taraka mwaka jana.