Redd’s
Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas akiwa ni mwenye furaha baada
ya kutajwa kuwa mshindi na kujinyakulia taji hilo baada ya kuwashinda
warembo wengine 11 katika kinyanganyiro hicho cha aina yake.
Redd’s
Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas katikati akipunga mkono kwa
furaha akiwa na mashindi wa pili Irine Veda (kulia) na Mshindi wa tatu
Joyce Baluhi mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa
shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa Septemba Septemba 1,
mwaka huu. Warembo hawa wote watashiriki shindano la Redd’s Miss
Tanzania 2012 baadae mwaka huu.
Washiriki
wa Shindano la Urembo la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012
waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya kutajwa kufanikiwa kupita katikia hatua hiyo. Kutoka kushoto ni
6. Zuhura Gora,
7. Irene Veda, 4. Salvina Kibona, 9. Rose Lucas na 5. Joyce Baluhi.
Add caption |
Warembo
wa Redds Miss Kanda ya Mashariki wakicheza show kali ya ufunguzi wa
shindano lao lililofanyika Hotel ya Nashera Mjini Morogoro usiku wa
kuamkia leo.
Wandaaji
wa mashindano ya Mikoa iliyoleta washiriki wa Miss Kanda ya Mashariki
wakitambiana huku Mwandaaji wa Mkoa wa Lindi, Ramadhan Shaha (katikati)
akionesha ishara ya ushindi aitumiayo mkiambiaji wa Kimataifa wa
Jamaika Bolt. Shaha alifanikiwa kutoa mshindi wa pili wa mashindano
hayo. Wengine kushoto ni Mwandaaji wa Mtwara, Rajab Mchata, Mwandaaji
wa Morogoro, Frank Ezekiel na kulia kabisa ni Mama Mchata.
....picha zaidi zitakujia muda si mrefu.