Na Mwandishi Wetu
MSHINDI
wa shindano la Bongo Star Search (BSS) 2009 Pascal Cassian atazindua
albamu yake ya nyimbo za injili iitwayo Yasamehe Bure kesho (Jumapili hii) katika Uwanja wa Fisi.
Albamu hiyo itakayokuwa na nyimbo kama vile Chuki ya Nini, Nikumbuke na Mimi, Jina la Yesu, Mafuriko, Pesa, Baba na Usilie.
Akizungumzia
albamu hiyo alisema kuwa ina lenga kuwarudisha waliopotea kwa Mungu kwa
kuwapatia ujumbe wa neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.
Alisema
kuwa akiwa kama kijana ameamua kutumia muda, nguvu na akili zake nyingi
katika kumwimbia na kumsifia Mungu na hivyo ameamua kuwafikishia
vijana, watoto na watu wazima ujumbe kupitia nyimbo.
Pia akizungumzia sababu ya kuzindulia albam yake katika eneo la uwanja wa Fisi alisema kuwa kutokana na
sifa mbaya ya eneo hilo ameamua ambapo limekuwa likifahamika kama
uwanja wa dhambi kutokana matukio mbalimbali ambayo yanafanyika mahala
hapo.
Alisema
kuwa mgeni rasmi anatarajia kuwa Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo
Star Search (EBSS) Ritha Paulsen ambae ndie alieibua kipaji chake
kupitia shindano hilo mwaka 2009 wakati likiitwa BSS.
Uzinduzi huo pia utasindikizwa na waimbaji wengine ambao ni Martha Mwaipaja, Sifa John, Joseph Kaka, Beatrice na wengineo wengi.
Albamu hiyo ambayo ameirekodia katika studio mbalimbali imemchukua miezi mienne kuiandaa na itauzwa kwa shilingi 10000/=.
“
Mimi kwanza ninamshukuru Mungu kwa kuniongoza mpaka kufikia hatua hii
ya kuzindua albamu yangu na ameweza kunifikisha hapa kupitia programu ya
BSS ambapo ndipo nilionekana uwezo wangu wa kuimba na kushinda na kumbe ilikuwa ndio mwanzo wa safari yangu ya kumtumikia Mungu” alisema Cassian