BAADA YA KUTOSWA KWA MIAKA MITANO MFULULIZO, HATIMAYE T.I.D APATA SHAVU LA KUPERFORM FIESTA YA DAR
Baada ya miaka mitano bila kupata nafasi ya kupanda kwenye stage ya
show za Fiesta, hatimaye Top in Dar, TID, atapanda kwenye show ya kilele
cha tamasha hilo la kila mwaka, litakalofanyika October 6 kwenye
viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam.Hiyo inamaanisha kuwa TID ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akijiita ‘Mnyama’ atashare stage moja na Rick Ross.
”KinoNdoNi+Fiesta+MnYaMA is equal to ‘Mtama wa ShiNGo’…..BhaaaaS
Watoto WadoGo mmekWiShA", ameandika TID ambaye jina lake ni Khalid
Mohamed kupitia Facebook.
Kupitia XXL ya Clouds FM, watangazaji wa kipindi hicho wamesikika
wakimtaja TID kama msanii rasmi atakayetumbuiza kwenye show hiyo.
Hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Facebook, hitmaker huyo wa
‘Kiuno’ alitoa malalamiko yake kwa kutokuhusishwa kwenye show hiyo kwa
muda mrefu.
“I wiSh I coUld maKe the Guy Who does the FieSta Listing be oN my
SiDe some PeoplE are workin verY Hard to juSt makE me Look like Criminal
so I can not be on List Lakini Mungu atanipa Better than Fiesta tho its
Been 5 years am nt Part of It,” aliandika.