-----
Kama
unakumbuka vizuri, miezi kadhaa iliyopita, baada ya kuandikwa kwenye
magazeti ya udaku kuwa anamsichana mwingine, na yeye kuruka futi mia na
kusema bado yupo na mpenzi wake wa kizungu "Suvi" ambae ndio kila kitu
kwake....
Leo hii Linex amethibitisha kuwa mambo yao hakuna anaeweza
kuyaingilia..ukimsikiliza kwa makini utagundua kuwa anajiami sana kwa
mpenzi wake huyo na ndo maana anajaribu kukuambia kuwa atakua ana
matatizo kama kuna kvuvi atakae weza kutupa nyavu baharini na kumvua
mpenzi wake wa sasa.
"kama
kuna mvuvi atatupa nyavu kumvua huyu shemeji yenu wa sasa hivi basi
ntakua nina tatizo, kwasababu maisha yangu mengi, nafkiri labda kwa
sababu ya the way i was living, sababu unajua mi nataokea mtaani sasa
labda the way nilivyokuwa naishi ilikua inafikia point watoto wa kike
wanachoka maisha yangu ya mtaani na nini, so wanaamua kunichoka na
wanaamua kuniacha na kuanza na maisha mengine,...
So hakuna jambo jipya
kwenye swala la kupenda kwangu mimi yaani ...mi sina kinyongo na mvuvi
ambae atatupa nyavu baharini na akafanikisha kumvua samaki ambae mi nilikua
napenda kumuona aendelee kuwa baharini akifanya maswala yake".