Mkurugenzi
wa kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed akibadilishana mkataba na
Msanii Diamond Platnumz baada ya kusaini. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria
wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo na
Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed ( kushoto) na msanii
Diamond Platnumz wakisaini mkataba wa kufanya kazi pamoja. Wanaoshuhudia
ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter
Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole
------------------------------------
MSANII wa
kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameingia mkataba
na kampuni ya I-View Studios ya ili wasimamie kazi zote kwa muda wa
miaka miwili.
Mkurugenzi
wa kampuni ya One Touch Solution ya mjini Dar es Salaam, Petter
Mwendapole amesema I-View itasimamia mikataba yote ya kazi zote za
msanii huyo na yeyote atakayetaka kufanya kazi na Diamond kwa sasa
itabidi awasiliane na I-View.
“Diamond
ameamua kufanya kazi zake kimataifa, na ameingia mkataba na I-View
ambapo wao ndio watakuwa wakisimamia maonyesho, matangazo, nyimbo kwenye
simu, nguo kila kitu ambacho kinahusiana nay eye kinapaswa kupitia
I-View,” amesema.
Mwendapole
alisema pamoja na maonyesho, lakini I-View pia itawajibika katika
muonekano mpya wa msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba ndani na nje ya
Tanzania. One Touch Solutions ndio watakuwa wasemaji wa msanii huyo.
Diamond kwa
upande wake alisema anataka kufungua ukurasa upya katika tasnia ya
muziki nchini na kwa anaamini utasaidia katika kumfanya aongeze nguvu
zaidi katika kutunga na kutengeneza nyimbo zake.
“Hii yote
ni kuhakikisha nafanya kazi zangu kwa ufanisi badala ya kujirundikia
mambo mengi, kuna watu walikuwa wakinitafuta wanashindwa kunipata lakini
sasa watakuwa wanafahamu ofisi ziko wapi na wanawasiliana na
menejimenti inawapa majibu, watu wa habari watakuwa na mtu wa
kuwasiliana nae moja kwa moja hata kama sipatikani,” amesema.
Diamond
anatarajia kutoa wimbo wake mpya ambao pia utarekodiwa na kampuni ya
I-View. Tayari usaili umeshafanuyika kwa ajili ya wale ambao wataonekana
kwenye video hiyo.