Kukataa Posho Ilikuwa Unafiki
Mbunge
wa Kigoma Mjini kupitia CCM Mhe Peter Serukamba amesema suala la baadhi
ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupinga posho
lilikuwa ni unafiki. Serukamba aliyasema hayo katika kipindi cha
Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango kupitia Magic FM. Fina aliuliza
moja ya swali kutoka kwa wasilizaji ambapo alisema biashara ya kukataa
posho ni unafiki tu huku akimwambia Fina ataje mbunge gani karudisha au
kukataa posho, alisema "Tumeongezewa mafuta tumechukua, tumeongezewa
vingine tumechukua hakuna ambaye amerudisha na next day ilipokuwa
confirmed wengine wakaanza kukopa" huku akisema hakuna umuhimu wa
kupinga posho za wabunge badala yake wabunge waombe serikali iwaongezee
posho na watumishi wengine.
Alipoulizwa kwa nini wasiiombe serikali ianze na sehemu nyingine kabla
ya kuwaongezea mshahara wabunge akitolea mfano wa shiri