MATENDO anayofanya mwanamitindo Jackline Patrick wakati mumewe
Abdullatif Fundikira akiteseka gerezani, yametajwa kuwa ni usaliti wa
asilimia miamoja na kwamba kama hatajirekebisha, mwisho wake utakuwa
mbaya.
Hayo yamekuja kufuatia hivi karibuni kupatikana kwa picha
zinazomuonesha mwanadada huyo akiwa kimahaba zaidi na modo mwenzake wa
kiume, Martin Kadinda huku mume wake akisota nyuma ya nondo.
Picha hizo zinawaonesha wawili hao wakiwa wamekumbatiana na kufanyiana mambo yasiyostahili kufanyika mbele za watu pale walipokuwa wakiogelea kwenye moja ya fukwe zilizopo jijini Dar na nyingine wakijiachia klabu.
HUYU NDO MUME WAKE AKIWA GEREZANI
HUYU NDO JACK AMBAYE NI "MKE WA MTU" AKILA BATA NA MWANAUME MWINGINE AMBAYE NI MARTINE KADINDA