MANECKY AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZINAZOMKABILI KUHUSU BEAT YA "DIAMOND" "NA PASHA"


Wakati wimbo wa Diamond ‘nataka kulewa’ ukitengeneza topic kwenye media kibao TZ na kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wengi wanasema beat hiyo inafanana asilimia 100 na ile ya beat ya wimbo wa Pasha alomshirikisha Tunda Man ‘Mtoto Amekua’, Manecky wa AM records ambae ndiye aliyetengeneza ‘nataka kulewa’ amesema beat ya wimbo huo ni tofauti kabisa na ile ya wimbo wa Pasha.

Producer huyo ambae ndiye mshindi wa kili music awards 2011 kama producer bora wa mwaka alifunguka kwa msisitizo kwenye XXL cha Clouds fm kuwa hakusample beat sehemu yeyote ile na hiyo beat aliifanya kwa mawazo yake mwenyewe kuanzia mwanzo kabisa.

Alipoulizwa maoni yake kama beat hizo mbili zinafanana au hazifanani, alisema “kwa kitu ambacho mimi nimeweza kusikiliza hizi ni beat mbili tofauti, sema kuna idea ya lead sound ambayo inaweza kuwa na mfanano flani, ndio maana nikarudia kusema palepale, mimi ni mtu ambae nasikiliza muziki kila siku, na ni binadamu na sio computer sio kitu flani ambacho kinasema ni kitu flani kifanye hivi…!”

Manecky amesema hata Tunda Man aliisikiliza ‘beat ya Nataka kulewa’ mara nyingi tu lakini hakuweza kuifananisha kabisa na ile ya wimbo wa Pasha ambao yeye mwenyewe kaweka vocal yake kwenye beat ileile inayofananishwa, lakini inaonekana alipousikia watu wanasema zinafanana ndipo na yeye akashtukia kuwa inawezekana iko hivyo.Duuuh..! 
 
Kweli tunatofautiana kushtukia copy, wengine wakisikia hata kinanda cha kwanza tu wanashtukia ila Tunda Man yeye ameshtuka baadae sana pamoja na kuitumia beat hiyo.

Wimbo wa Diamond umepata challenge kubwa sana tangu au-release rasmi, muda mchache baada ya kuonekana beat inafanana na ya wimbo wa Pasha ft. Tunda Man ‘nataka kulewa’, H-Baba alijitokeza na kumtuhumu Diamond kwa kumuibia idea ya wimbo huo tena kwa makusudi huku akiweka hadharani vielelezo vya demo ya wimbo wake ‘nataka kulewa’ akiwa na Q-Chillah.