Mpiga picha akiibukia kwa chini ya Shilole kutafuta “utupu”
Mpiga picha alikaa kwenye “angle” gani ili kupata picha kama hii?
Nini kimenifanya nizungumzie hili?
Kuna picha za Shilole ambazo ni mfano mzuri sana wa skendo feki, skendo za kulazimishia. (angalia picha hizo chini.) Picha hizo zilisababisha blogs kujaa na vichwa kama:
“Aibu tupu: Shilole naye amwaga radhi kweupeee!”
“Shilole yaye azianika nyeti zake”
“Shilole akaa mtupu jukwaani”
“Shilole nae aacha sehemu zake za siri wazi jukwaani”
Na nyingine nyingi kama hizo. Ukiingia kusoma wanavyochana ndio utachoka kabisa! Lakini ukweli ni kwamba hili si kosa la Shilole. Bali mpiga picha alipania kupata picha za “skendo” kwa udi na uvumba. Kwanini nasema hivi?
1. Gauni aliyovaa Shilole, ni kawaida tu wala siyo “scandalous” kwa night club au concert; na pia alivaa nguo za ndani za kujisitiri vizuri “in case of accident.”
2. Angalia kwa makini “angle” aliyoitumia mpiga picha utagungua kwamba hii ni skendo feki ya kulazimishia. Utagundua kwamba mpiga picha huyo alipiga picha kutokea chini ya alipo Shilole akiangalia juu kwa makusudi ili apate picha za “utupu.” Kwa angle aliyotumia mpiga picha huyo, angepata picha ya nguo za ndani za mwanamke yoyote hapa duniani aliyevaa sketi au gauni isiyovuka chini ya magoti. Alichofanya mpiga picha huyu imenikumbusha ile tabia ya kitukutu tuliyokua nayo utotoni katika shule za msingi; tabia ya kuweka kioo chini ya wanafunzi wakike waliovaa sketi ili uone rangi ya chupi zao halafu uanze kuwatania. Tofauti ni kwamba hawa wanaofanya hivi si watoto, bali ni watu wazima na akili zao timamu wanaofanya hivi wakijua watatengeneza fedha kupitia “schadenfreude” tuliyokua nayo Watanzania kwa mastaa wetu.