Aliongeza kuwa licha ya kifo cha mtoto huyo, baba mmoja aitwaye Mtimba Manyeye (64) naye alipoteza kidole cha mkono wa kushoto baada ya kushambuliwa na mamba akiwa kando ya Ziwa Victoria.
Aidha, Afisa Mtendaji Ndaro alisema wanyamapori wamekuwa wakisumbua wananchi na akatoa mfano wa nyani ambao wapo zaidi ya 1,000 nao wamekuwa wakisumbua sana wakulima wa eneo hilo kwani wameharibu zaidi ya hekari 150 za mashamba yao, hivyo kuwafanya kukata tamaa kuendelea kulima.
“Maofisa wa wanyamapori wamekuwa wakifanya msako lakini wanyama hao wanaendelea kuwa tishio kwa raia,” alisema Ndaro.