Shindano la kuwasaka wasanii wasanii bora 10 kati ya 25 walioingia katika mchuano wa kusaka tuzo maalum ya mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kupitia shindano lake alililibuni na kulipa jina la kabati katiba Star Serach limefanyika leo katika ukumbi wa Twistars mjini Iringa.
Msigwa amesema kuwa awali wasanii walikuwa
wakionyesha uoga katika jukwaa ila kwa sasa wameonyesha
kujiamini zaidi.
Aliwataja wasanii walioingia hatua ya
fainali leo kuwa ni Alfred Madembwe,Adimaya Mlawa,Humphrey
Sambala,Mohamed Mpangala, Jackson Mam,Henry Said, Edga Bosco , Emmanuel
Mgata , Julius Kimata na Adam Kayombo.
Huku Jaji mkuu wa shindano hilo Edo Bashir akieleza
kufuruhishwa kwake na jinsi ambavyo wasanii hao wanavyojituma
katika jukwaa na kuwa upo uwezekano wa mkoa wa Iringa
kupitia shindano hilo kutoa wasanii bora zaidi ambao
wanaimba vizuri kuliko hata wasanii wakubwa hapa nchini.