FILAMU YA UJINGA WANGU NI MOTO MKALI

Mtayarishaji wa filamu Bongo Paul Mtendah anasema kuwa filamu yake mpya inayoitwa Ujinga wangu inayotarajia kuingia hivi karibuni sokoni itakuwa ni filamu ya aina yake kutokana na kuitengeneza filamu hiyo baada ya kuhitimu masomo yake ya uongozaji wa filamu Chuo Kikuu Idara ya Sanaa siku chache na kujifunza mambo mengi ya filamu.“Tasnia ya filamu ya inazidi kukua na inahitaji ujuzi zaidi kwa kuliona hilo nilishiri kusoma masomo ya uongozaji filamu {Directing Course} na baada ya kumaliza kilichofuatia ni kuamua kutengeneza filamu hii ya Ujinga Wangu, filamu inayojaribu kuongelea masuala ya mahusiano na migororo ya kifamilia ni filamu yenye ujumbe na ubora pia,”

  Filamu ya Ujinga wangu imewashirikisha wasanii nyota katika tasnia ya filamu nchini kama vile Yvonne Cherryl ‘Monalisa’, Hemed Suleiman, Mboto, Vanitha Omary,na wasanii wengine wanaotamba katika tasnia ya filamu, filamu hiyo imeongozwa na Paul Mtendah ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu hiyo.