Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuwasili akiwa sambamba na skwadi lake zima la Quartier Latin kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),tayari kwa onesho lake litakalofanyika siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba.....
Onesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Afrika Masharikia (EABL) kupitia kinywaji chake cha Tusker kiingilio chake kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= kwa kichwa kama tiketi ikinunuliwa mapema na shilingi 15,000/= getini.Pichani kushoto ni Mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza na (mgeni wake) ,Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar usiku wa kuamkia leo
Baadhi ya wanamuziki wa Koffi Olomide wakishuka kwenye gari kwenye viunga vya hoteli ya Serena usiku wa kuamkia leo .
Baadhi ya wadau na wapenzi waliokumbana uso uso kwa na mwanamuziki Koffi Olomide usiku wa kuamkia leo,wakipata picha ya pamoja.
Mdau Idd Janguo nae alipata picha ya ukumbusho na Koffi Olomide,ambaye anasema amejipanga vyema kuwaburudisha wakazi wa jiji la Dar siku ya jumamosi ndani ya vuwanja vya Lidaz Club.