Diamond Platnumz, jina ambalo litaendelea kuwaumiza vichwa watu wengi
hasa wasanii wenzake ambao wanaitamani nafasi aliyoshika yeye kwa sasa,
the dude is running this game kwa sasa kiukweli na ni ngumu sana kuamini
kwamba atashuka kiwango soon.
Haujapita muda mrefu since ameachia video kali ya 'Nataka Kulewa', leo
hii anazidi kuwachanganya akili fans wake kwa kudrop another big thing
another brand new video "KESHO" ambayo kwa kuitazama tu inaashiria ni ya bajeti na maandalizi ya kutosha.
This time around Platnumz hajalia kama ilivyokuwa katika nyimbo zake
zilizopita lakini bado yuko kwenye duara la mapenzi, akimwambia mbaibe
wake kuhusu siku ya Kesho ambayo wanapanga kwenda kwa wazazi.
Video hii imefanyika nchini Kenya chini ya Ogopa Videos, na video girl
katika video hiyo ni msanii mkubwa wa kike wa Kenya Avril. Master
Mastar wengine wakubwa wwa Kenya walioonekana kwenye video hiyo ni
pamoja na William Tuva mtangazaji wa Citizen Radio/TV, Collo, na Colonel
Mustafa.