MAHACKER WAIOBOMOA WEBSITE YA PROFESA JAY.....TEMBELEA UJIONEE




Watu wanaosadikika kuwa ni wahuni wa kitechnolojia wameonekana kutenda mambo yao katika Official website ya Daddy wa muziki wa rap Tanzania, Proffesa Jay http://www.professorjaytz.com/  ambayo kwa mujibu wake mwenyewe, site hii ilikuwa bado ipo katika matengenezo na kuna mtu maalum ambaye alikuwa amemuasign kazi ya kuitengeneza.
Hivi ndivyo site ya msanii huyu inavyoonekana kwa sasa;
Jay mwenyewe ambaye hadi wakati tuliokuwa tunaongea naye alikuwa hafahamu kuhusiana na kutokea kwa issue hii, amewaahidi mashabiki wake kulifuatilia swala hili na kuhakikisha anaweka kila kitu katika mstari.

Rapa huyu mchana wa leo atakuwa akitoa Burudani pande za Chuo kikuu Cha Dar es Salaam katika Kongamano maarufu la Kigoda Cha Mwalimu Nyerere kwa mwaka huu, Kongamano ambalo limeanza jana na linatarajiwa kuisha siku ya kesho likiwa na kauli mbiu 'Maendeleo ni Mapambano ya Ukombozi'.