RAY ASALIMU AMRI BAADA YA KUKUBALI KUACHANA NA FILAMU YAKE ILIYODAIWA KUWA INA UDHALILISHAJI MKUBWA
Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
HATIMA ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sister Mary iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.
Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama Polycarp Kadinali
Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa
ikionesha udhalilishaji kwa namna ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.
Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Ray amebainisha kuwa baada ya
kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye filamu hiyo, ameona ni bora
kuachana nayo kwani hata akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya
wakati mwingine.
“Asilimia 85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo
walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa nimeanza kushuti filamu
nyingine kabisa ile labda nije kuirudia upya hapo baadaye,” alisema Ray.