Rapper
Ilunga Khalifa aka Cpwaa amesema uamuzi wa Tanzania kuhama kutoka
kwenye mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda wa digitali umewapa
changamoto kubwa wasanii wa muziki Tanzania kwakuwa wananchi wengi sasa
wana uwezo wa kuona channel nyingi za kimataifa zinazocheza video kali.
Akizungumza kwenye kongamano kuhusu mchango wa technolojia ya
mawasiliano na habari, ICT kwenye tasnia ya burudani nchini
lililofanyika juzi Jumatatu katika kituo cha ubunifu wa ICT cha KINU
jijini Dar es Salaam, Cpwaa alisema wasanii wakiendelea kufanya video
zao kwa mazoea zitaishia kuchezwa hapa hapa nchini na kushindwa
kufaidika na mfumo huo.
““The sad story you used to see EATV, Clouds TV, EATV, DTV, Channel 1O,
C2C but right now you have Trace TV, BET so the viewers right now are
exposed to more advanced television and the say like I ain’t gonna watch
that ….. cause they didn’t afford DSTV and stuffs like that,”,”
alisema Cpwaa.
Ameongeza kuwa wasanii sasa wanatakiwa kujipanga sababu wananchi
wengi wana uwezo wa kuona vituo vingine kama Trace kupitia ving’amuzi
hivyo ni lazima wafanye video zenye viwango ili nyimbo zao zichezwe huko
pia.
Hizi ni baadhi ya picha ya Kongamano hilo lililofanyika kama sehemu ya Mobile Mondoy (MOMO) hapo KINU.