Halima Mdee Amvaa Tibaijuka




TAARIFA KWA UMMA

MHE. TIBAIJUKA, NI WAKATI WA VITENDO SASA PUNGUZA MANENO

KWA nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,

nimefarijika na kauli ya serikali iliyotolewa karibuni na Waziri wa Ardhi , Nyumba


Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi

Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya

zilizojengwa kando kando ya fukwe

Huvisa kwamba nyumba zote

za bahari

kutokana na kukiuka Sheria za Ardhi na Mazingira za

mwaka 1992, 1995 na 2004.

Pamoja na kufarijika huko, nimelazimika kutoa taarifa hii kwa umma ili

kuwakumbusha wahusika na hususan mawaziri husika sasa wathibitishe uwezo

wao na dhamira zao kuwatumikia Watanzania kwa kuwajibika kwa vitendo.

Si maneno. Nasema haya kwa sababu imekuwa ni kawaida sasa kwa viongozi

waandamizi serikalini kuwa ’wazuri’ wa kutoa matamko ya kisiasa, lakini

wanapatwa na kigugumizi cha hali ya juu unapotakiwa utekelezaji wa vitendo! Hii

pia inachangiwa na ukweli kwamba vyombo vya dola vinavyopaswa kusimamia

utekelezaji wa maagizo mbali mbali ya serikali kutawaliwa na rushwa na uzembe

Ninayarejea haya kutaka tu kuukumbusha umma wa Watanzania ili wawe

makini kufuatilia uwajibikaji wa serikali kwa wananchi. Itakumbukwa kwamba

kuwa chanzo cha matamshi hayo ya mawaziri, Prof. Tibaijuka na Dkt. Huvisa ni

matokea ya ziara iliyofanywa na Waziri wa Ardhi, Jimbo la Kawe, Kinondoni, Dar

es salaam. Ziara ambayo ilishuhudia pasipo kificho, namna ambavyo watu wenye

nguvu ya fedha wanadiriki kuharibu mazingira kwa makusudi pasipo kujali athari

ambazo zinaweza kutokea sasa na baadae kwa wakazi wa maeneo jirani na Taifa

Ninasema kwa makusudi kwa kuwa baadhi ya majumba makubwa yaliyojengwa

maeneo yasiyoruhusiwa tuliyoyatembelea, yanamilikiwa na viongozi wakubwa

Lakini pia kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya

Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kawe kwa kushirikiana na NEMC, Naibu Waziri

wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Ole Medeye na maofisa wa

ngazi za juu wa Wizara ya Ardhi na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa

nyakati tofauti tulitembelea maeneo yanayotolewa maagizo sasa hivi yakiwa

katika hatua ya awali ya ujenzi wa msingi! Leo ni mengine ni majengo makubwa

Ndio maana nadiriki kusema yaliyozungumzwa na mawaziri hao sio mapya!

Hata kidogo. Nasisitiza tena, wawajibike kwa vitendo kwa kuchukua hatua

ambazo ziko ndani ya uwezo wa serikali. Si maneno. Nitatoa mifano michache ,

ambayo kama ingefanyiwa utekelezaji kama amri za serikali zilivyoelekeza hapo

awali ,ingetosha kuwa fundisho kwa wengine wote ambao wanadhani nguvu yao

ya fedha inaweza kuwafanya wawe juu ya sheria na mstakabali wa Watanzania!

1) Mwaka jana 4/1/2011 Wizara ya Ardhi kupitia barua yenye kumbukumbu

namba LD/297571/18 waliandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri

ya Manispaa ya Kinondoni kuhusiana na uvamizi wa kiwanja nana 2019 na

2020 Mbezi Kawe . Katika barua hiyo pamoja na mambo mengine ilibainisha

kwamba wizara imefanya ukaguzi katika viwanja tajwa hapo juu baada ya

kupata malalamiko juu ya uharibifu wa mazingira unaoendelea katika eneo

hilo. Barua husika inabainisha kwamba ukaguzi walioufanya umeonesha

unaofanyika katika eneo husika, ambalo kwa mujibu wa

Tangazo la Serikali (GN) No. 76 ya mwaka 1992 uendelezaji unaofanyika

hauruhusiwi. Kisha ilimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuchukua hatua za

kubomoa/kuondoa uendelezaji batili unaofanyika katika viwanja Na 2019 na

2020 Mbezi Kawe. Barua husika ilisainiwa na bwana Sadoth K. Kyaruzi, kwa

niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara.

Tangu barua hiyo iandikwe na kuelekeza hatua zichukuliwe, leo mwaka 1 na

miezi 5, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. Taarifa za uhakika na ukweli

zilizopo, ni kwamba ubomoaji ulikwama mara kadhaa kwa sababu National

Management

Council (NEMC) pamoja nna Mkurugenzi wa

Manispaa ya Kinondoni walikosa ushirikiano kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa

Kinondoni! Wasingeweza bomoa pasi na ulinzi! Kuna harufu ya Rushwa.

barua ya tarehe 30/9/2011

kwa Bwana Frank Mushi. Barua husika, ilitoa maelekezo kwa Bwana Mushi

kuvirudisha katika hali yake ya kawaida, viwanja namba

mujibu wa vifungu 55(2) (a) (e), (3) na 151 (1) ,(2) (a), (b), (3) ,(4) (b) na

(f) vya Sheria ya Mazingira, sura 191 ya mwaka 2004.

Barua husika inabainisha kwamba timu ya

Mazingira (NEMC), Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara

ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Halmashauri ya Jiji la Dar

es salaam na Manispaa ya Kinondoni ilitembelea eneo husika kufuatia

malalamiko kutoka kwa viongozi na wakazi wa Kawe Beach. Timu hiyo

ilibaini kwamba mto Ndumbwi, pamoja na bahari ilikuwa inajazwa mawe

na vifusi hali iliyosababisha kupatikana kwa viwanja na 2019 na 2020.

Ambapo ndani ya viwanja hivyo lilikuwa linajengwa jumba kubwa kinyume

kabisa na vifungu 55(2)(a) , 55(2) (b) , 55(2)(d) na 55(2)(e) vya Sheria

ya Mazingira.Pia ilibainika kwamba mikoko ilikatwa kinyume na s.63(1) ya

Kwa mujibu wa nyaraka nilizonazo, yafuatayo yalijitokeza

i) timu ya wataalam ilibaini kwamba, tayari Wizara ya Maliasili na Utalii

ilishatoa zuio la ujenzi katika kiwanja husika.

ii) Manispaa ya Kinondoni, mara kadhaa iliweka zuio la uendelezaji na kutoa

amri kwa ’mmiliki’ wa eneo husika kubomoa, lakini mmiliki huyo

alipuuza amri hiyo na kuendelea na ujenzi! Taarifa zilizopo Bwana

Mushi yupo kama chambo. Nyuma yake kuna kiongozi mkubwa

Serikalini. Ukifika wakati mwafaka tutamtaja. Hasa iwapo viongozi

husika wataendelea ’kuwauzia’ wananchi maneno badala ya vitendo.

iii) Ilitolewa amri ya Mahakama, tarehe 5/4/2011 kumtaka Bwana Mushi

asiendelee na ujenzi. Bwana Mushi aliipuuza amri husika na kuendelea

Baraza la Mazingira lilimwagiza tena, Bwana Mushi:-

1) Kuacha ujenzi mara moja

2) Kuvunja majengo yote yaliyoko kwenye viwanja vyenye mgogoro

3) Ndani ya siku saba, tokea amri husika kutolewa (amri ilitolewa 30/9/2011)

awe ametoa mawe na vifusi vyote vilivyoharibu mkondo wa maji na bahari

na kuurudisha mto na bahari katika hali yake ya kawaida.

4) Ndani ya siku 30 chini ya usimamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii

kuhakikisha kwamba mikoko yote iliyokatwa imerudishwa katika hali

iliyokuwa awali. Kwa gharama za Bwana Mushi.

Hakuna kitu chochote kilichofanyika! Ujenzi umeendelea, nyumba imekwisha,

mto, bahari na mazingira kwa ujumla vimeharibiwa vibaya! Juu ya sheria. Juu

ya maslahi ya wananchi wa eneo husika na Watanzania.

3. Nyaraka nyingine ni Taarifa ya Uchunguzi wa Mgogoro wa Ardhi na Mazingira

katika eneo la Kawe Beach. Taarifa hii ilitolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais,

Agosti 2010 kufuatia kuundwa kwa kikosi kazi kuchunguza uhalali wa viwanja

namba 1040, 1041, 2000, 2002 na 1071. Chanzo cha mgogoro husika

kubuniwa kwa viwanja vya nyongeza kando kando ya Mto Mbezi katika eneo

linaloelekea baharini, hali inayopelekea

mazingira na makazi ya wananchi walio jirani na eneo hilo! Kamati ilifanya kazi

yake na kutoa mapendekezo mazuri yenye lengo la kuokoa mazingira! Tangu

mwaka 2010 hadi leo hakuna kilichofanyika!

maji ya mto kutuama na kuharibu

Kitu kinachoshangaza na kusikitisha ni UJASIRI na WEPESI wa kutoa matamko,

kuunda kamati au vikosi kazi, lakini vikosi kazi baada ya kufanya kazi yake,

linapokuja suala la utekelezaji wahusika, wakiwemo mawaziri wanapatwa na

vigugumizi. Haijulikani wanakopata pia ujasiri wa kutoa visingizio wakati sheria

Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, Sura 191 ya mwaka 2004, Fungu 57(1)

hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kudumu za kibinadamu ndani ya mita

60 ambazo kwa asili yake zinaweza kuhatarisha au kuathiri vibaya ulinzi wa

mazingira na utunzaji wa bahari au kingo za mto, bwawa au mwambao wa asili

wa ziwa. Halikadhalika, Sheria

Fungu 7 (1) (d) inabainisha kwamba eneo lolote lililo ndani ya mita 60 kutoka

kingo ya mto na bahari linatakiwa kutangazwa kama ardhi hatari au kuhifadhiwa.

ya Ardhi Na. 4

Pale inapotokea kuwa masharti ya Sheria moja yanapingana

Sheria ya Mazingira, kuhusu mambo yanayohusu usimamizi wa Mazingira, Sheria

ya Mazingira ndiyo hutumika, kwa mujibu wa Fungu 232 la sheria ya mazingira

Ndio maana nasisitiza! Hatuna haja ya kutoa matamko! Walio na mamlaka,

waliokabidhiwa dhamana, sasa tufanye kazi kwa vitendo! Haitoshi tu kutamka

maneno makali ya kisiasa, wananchi wanataka kuona uwezo wenu dhahiri

kwenye kuchukua hatua, tena zilizoko ndani ya uwezo wenu kisheria. Si

Nadhani ni wakati muafaka sasa kwa Waziri wa Ardhi , wakati akijiandaa kuvunja

majumba yote yaliyojengwa ufukweni kufanya tathmini yale aliyokwisha yatolea

matamko huko nyuma, yamefanikiwa kwa kiwango kipi! Namkumbusha hili

sambamba na ahadi zake kwa Watanzania za kurudisha viwanja vya wazi vyote

vilivyovamiwa. Zoezi ambalo limekuwa likienda kwa kusuasua sana! Awaambie

amefikia wapi au anakwamishwa na nini kilicho juu ya sheria na maslahi ya

Tunataka viongozi wa serikali waelewe kuwa Watanzania wamechoka na maneno

na ahadi za kila siku ambazo hawaoni utekelezaji. Wanataka ’kuuziwa’ matendo
 
Halima Mdee
Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi