Zitto Kabwe: Sheria Inayowanufaisha Waghana Na Gesi Yao
Sheria ya Usimamizi wa Mapato za Mafuta na Gesi ya Ghana (Petroleum Revenue Management Act 2011) ni nzuri sana. Waziri wa Fedha aliahidi kwenye 'letter of intent' kwa IMF kwamba tutatunga sheria kama hiyo ifikapo mwisho wa mwaka. Nadhani sheria hii inaandikwa kwa siri sana maana imekuwa kimya sana. Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi Asilia inapaswa kuwa wazi kuanzia matayarisho ya kuandikwa kwake mpaka katika utekelezaji wake. Uwazi na Uwajibikaji ni dhana muhimu sana katika kuhakikisha Taifa linafaidika na utajiri wa Mafuta na Gesi na Nchi kuepuka laana ya Mafuta (Oil Curse).- Zitto