MARIAH CAREY AZUNGUMZIA BIFU LAKE NA NICKI MINAJ



Mariah Carey
Kumekuwepo rumors zilizozagaa kwenye mitandao kuwa kuna beef la chini chini kati ya Mariah Carey na Young Money rapper Nicki Minaj, ambao wote ni majaji wa American Idol.
 
 Rumors hizi zilianza tu baada ya Nicki Minaj kutangazwa kujoin team ya majaji wa AI, ambapo ilisemekana Mariah Carey hakupenda kabisa ujio wa Nicki Minaj kama jaji wa AI na ikasemekana kuwa Mariah carry alipopigiwa simu kuambiwa kuwa Nicki anajoin American Idol alikata simu baada ya kusikia hiyo message.

The R&B diva Mariah carry amefunguka kuhusu uvumi huu ili kuweka mambo sawa kwa sababu ukimya wake ulizidisha kusambaa kwa rumors hizi. 
 
Na ameonekana kutochukulia hizi rumors seriously, “How they could have sparked a feud in such a short time span?” 
 
Mariah aliuliza kwa shangao kwa sababu mashindano yenyewe yana siku mbili tu na huu muda ndo unamfanya Mariah aulize mara mbilimbili inakuaje chuki isambae hivi ndani ya siku mbili, “a feud takes a little longer to spread out, than that” alisema Mariah Carey huku akitabasamu.

Nick Minaj
Katika siku ya kwanza ya audition iliyofanyika New York City, MTV iliwatembelea majaji hao ili kuona kilichokuwa kinaendelea na MTV iliwashuhudia majaji hao wakitabasamu na kuwapokea vizuri tu, na walipoulizwa kama ni kweli wanabeef wote walicheka na Mariah Carey alimaliza kwa kusema “it’s fun, it’s music, it’s singing, it’s laughter.’’
 
  Wakati huo Nicki yeye alitikisa kichwa na akaonekana anachekeshwa na hiyo rumors ya beef.

Hata hivyo camera za MTV zilinasa jinsi ambavyo audition ilivyokuwa pale New York City, na mara nyingi kullikuwa na mabishano kati ya Nicki Minaj na Mariah Carey, wakati Nicki Minaj alipotoa comment zake kuhusu alichofanya contestant, Mariah Carey aliingilia, na Nicki Minaj alimjibu Mariah kwa sauti ya juu sana.
 
Ripoti kutoka kwa Spy wa American Idol zinasema kuwa majaji hao wanajaribu tu kuficha tofauti zao lakini kila mtu aliona wazi kabisa kupitia hiyo audition ya kwanza pale NYC.

Haya sasa siku mbili tu haya yote yamesikika, au kwa kuwa wote ni wasichana wenye majina makubwa, hili zizi moja la AI litakalika hadi mwisho watakapomaliza audition za Nchi nzima?