Kijana ambae amekuwa akiwaliza watumishi mbalimbali wa umma na watu binafsi
kwa kutumia jina la waziri wa
nchi ofisi ya waziri mkuu
sera na uratibu wa bunge kijana
Jonathan Wiliam Lukuvi( si jina lake halisi)amekamatwa katika hafla ya kanisa
la Overcomers FM akitaka kumtapeli waziri mkuu
wa zamani Edward Lowassa kupitia
harambee hiyo.
Kijana
huyo aliingia katika ukumbi wa St.
Dominic leo katika harambee ambayo
mgeni rasmi alikuwa ni Lowassa na kupita mbele na kutumia kipaza
sauti
kuzungumza kuwa anaitwa JOnathan
Wiliam Lukuvi na ni mtoto wa
waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na kuwa
amekuwa akimpigia simu mara kwa mara Lowassa na hata katika mkutano
wake
wa Jangwani jijini Dar es Salaam
alipata kuzungumza na Lowassa na hivyo kuomba
kutekelezewa ombi lake la msaada
ambao hakuutaja.
Kutokana
na
utambulisho huo baadhi ya
watu waliopata kutapeliwa na kijana huyo akiwemo mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa waliweza kuguna hali iliyopelekea
askari
polisi kufunguka na kumtia
mbaroni kijana huyo ambae alikuwa akiweka mtego wa kumtapeli
Lowassa na viongozi
wengine katika hafla hiyo .
Hata hivyo baada ya
polisi kumtia nguvuni kijana huyo
baadhi ya watu waliotapeliwa
waliweza kumtambua huku familia ya Lukuvi iliyokuwemo katika ukumbi huo
ikimkana katu katu kuwa hana hata
chembe ya familia na watu
hawamtambui .
Kada wa CCM
maarufu mkoani Iringa Godfrey
Malenga Lukuvi alisema
kuwa kijana huyo
amekuwa akitumia jina la waziri
Lukuvi kuliza watu na kuwa wengi wamekuwa
wakilalamika kuhusu utapeli
unaofanywa na kijana huyo na kuwa
tayari alipata kukamatwa na polisi ila
alitolewa .
Kwa upande wake
katibu wa mbunge jimbo la Isimani ambae pia ni familia ya Lukuvi Bw
Thom Malenga Lukuvi alisema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mbali mbali
kutoka kwa watu mbali mbali ambao
wamelizwa na kijana huyo na
kuwa siku zote
alikuwa akiweka mtego ili kumnasa kijana
huyo tapeli japo
hakufanikiwa kumpata.
Thom ambae
yupo nje ya mkoa wa Iringa
kwa shughuli za kifamilia alisema
kuwa alitamani sana kama
angebahatika kumshuhudia kwa macho
kijana huyo tapeli ila kwa kuwa
yupo nje ya mkoa atajitahidi
kurudi mapema mjini Iringa ili kumwona
tapeli huyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo alimweleza mwandishi wa mtandao
huu wa www.matukiodaima.com kuwa
pia kijana huyo alipata kufika
ofisini kwake kwa ajili ya kumtapeli na baada ya kumshtukia alimtafuta waziri Lukuvi kwa simu na kuelezwa kuwa kijana
huyo ni tapeli mkubwa .
Hata hivyo mwanahabari
Gerald Malekela wa radio Nuru
Fm alisema kuwa kijana huyo alipata
kufika studio za radio
hiyo kwa ajili ya kutapeli uongozi kwa
kutumia jina hilo na kufika studi
za radio hiyo huku akiwa na barua inayosifia watangazaji na kuomba kusaidiwa
zaidi kama mmoja kati ya
wasikilizaji .
Mtandao huu
ulipata nafasi ya kumtafuta kwa
njia ya simu waziri Lukuvi ambae
mbali ya kumkana kuwa
hamtambui bado alisema kuwa amepata
kuwaliza watu mbali mbali
kwa kutumia jina lake.
Lukuvi alisema kuwa tayari amepata kupokea malalamiko kutoka kwa
mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa na kumwagiza
kumtakata na kutaka sheria ichukue mkondo wake.
"Mimi
huyu kijana simtambui na
wala si ndugu yangu ila amekuwa
akitumia jina langu kutapeli watu na
tayari alikamatwa na polisi kwa
utapeli huo"
Mkuu
wa mkoa wa Iringa
Dk Christina Ishengoma aliwaonya watu
wanaoendelea kutapeli wengine kwa
kutumia majina ya viongozi ama namna nyingine yeyote kuacha mara moja
na kuwa akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
hatakubali kuona matapeli hao wakiendelea
kulizwa watu kwa njia ya
udanganyifu .