Mamlaka
ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA) imetoa taarifa usiku huu juu
ya ujumbe mfupi wa simu uliokuwa ukisambazwa kwa watumiaji wa simu za
mikononi hapa nchini uliokuwa ukieleza kuwa ifikapo saa tano usiku (kwa
masaa ya Afrika Mashariki) watumiaji wa simu hizo wanatakiwaa kuzizima
simu zao kutokana na mionzi ya Sarari moja ambayo ingepita karibu na
Dunia na ambayo inasemekana kutokana na mionzi hiyo watu watumiao simu
hizo wangeweza kupoteza maisha au kupatwa na madhara makubwa kama
wasingekuwa wamezima simu zao.
Mamlaka
ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA) imekanusha vikali taarifa
hizo na kusema taarifa hizo ni za uongo na kuifananisha taarifa hii na
ile ya miaka kadhaa iliyopita ilikuwa ikisema kuwa kuwa makini na
ujumbe mfupi wa mionzi.
TCRA
imewataka wananchi woote na watumiaji wa simu za mkononi
nchini,kuzipuuza taarifa hizo kwani hazina ukweli wowote na zimeanzishwa
na mtu ambaye hana lengo zuri kwa watumiaji wa simu za mikononi.