“Unajua mama Ray hampendi Mainda, aliwahi kumwambia Ray kuwa, asimuone msichana huyo nyumbani kwake kwani anahisi yeye ndiye anayumbisha maisha ya mwanaye,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya ishu hiyo kutua kwenye dawati la Risasi Mchanganyiko, waandishi wetu waliingia mzigoni na kumwendea hewani Mainda na kummwagia upupu na hivi ndivyo ilivyokuwa;
Mwandishi: Haloo Mainda!
Mainda: Haloo dada, unasemaje?
Mwandishi: Kuna habari zimetufikia zinasema kuwa hukubaliki ukweni.
Mainda: Jamani sipendi kuongelea mambo hayo kabisa, kwanza nipo shooting.
Baada ya mazungumzo hayo, mwandishi wetu alikata simu na kumtafuta siku iliyofuata ambapo mazungumzo yalikuwa marefu huku Mainda akiahidi kufika ofisini kwetu ili kutoa ufafanuzi.
Hata hivyo, Mainda alidharau na kuendelea na kazi zake ambapo waandishi hawakukata tamaa walimwendea hewani siku mbili zilizofuata na mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo.
Mwandishi: Haloo Mainda!
Mainda: Niambie dada.
Mwandishi: Mainda inasemekana wewe na mama mkwe wako hampatani, anadai wewe unamsababishia mwanaye kuyumba kimaisha kwa mambo ya kindumba, unaliongeleaje hilo?
Mainda: (huku akiangua kilio) Jamani, jamani hivi ni nani anayewaleta habari mbaya hivyo, kwanza mimi sijawahi kwenda kwa mganga hata siku moja, nimeokoka na siwezi kufanya hivyo.
“Ninajua wanaoleta habari hizo ni Bongo Movies, sijui nimewakosea nini lakini nakuja ofisini kwenu mniambie hao watu kwani wananichukia na ninyi mnawalea.”
Baada ya Mainda kuzungumza hayo, habari ilisitishwa na kumsubiri Mainda afike ofisini kwetu lakini hadi tunaandika habari hii zilipita siku mbili bila staa huyo kufika ofisini kama alivyoahidi.