Anikulapo Kuti akiwa na wake zake watatu wakati wa ndoa yao.
FELA
Anikulapo Kuti, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ametoa
mpya kwa walimwengu kwa kufunga ndoa na wanawake watatu.Mtu huyo ambaye anatumia jina la mwanamuziki aliyevuma zamani wa
Nigeria, hayati Fela Anikulapo Kuti, amefunga ndoa hiyo kufuatia
mchungaji wa kanisa lake nchini humo kuwaambia waumini wake kwamba
wanaweza kuoa wanawake wengi, jambo ambalo limeleta mkanganyiko mkubwa
kwa waumini wa madhehebu ya Kikristo barani Afrika.
Ndoa hiyo ilifungwa kama kawaida, ambapo watu hao wanne waliapa kuwa mume na wake zake, wakishuhudiwa na watu kibao huku kiongozi aliyeifungisha ndoa hiyo akinukuu vifungu vya Biblia ambavyo hutumiwa na Wakristo wote.
Tukio hili limeleta mkanganyiko mkubwa na kuwaacha watu wengi wakijiuliza mengi kuhusu madhehebu ya Kikristo yanavyojiingiza katika matendo yasiyoendana na imani yao, ambayo inasisitiza mke au mume kuwa na mwenza mmoja tu.
Chanzo: www.informationnigeria.org