Msanii
wa filamu nchini Mohamed Nice ‘Mtunisi’ (kushoto) na Jacob Steven ‘JB’
wakiwa katika duka ambalo lilikuwa linauza kazi zao ambazo ni feki
ambapo watuhumiwa walikamatwa kwa kushirikiana na Kampuni ya usambazaji
ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam
Baadhi ya watu wakiwa wamekusanyika kushudia ukamatwaji wa kazi za wasanii mtaa wa Magili na Likoma jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Mizigo ya Dvd mpya kabisa zilizo feki zikiwa zimekamatwa.
Wasanii
Mzee Yusufu (kushoto) na Mohamed Nice wakiwa Katika Duka lililokamatwa
kwa kuuza kazi Feki za wasanii. Msako huo uliwashirikisha kampuni Ya
Steps Entertainment pamoja na wasanii wenyewe
Mtuhumiwa wa Kurudufu kazi za wasanii akihojiwa na ITV huku akiwa Chini ya Ulinzi baada ya Kukamatwa.
Baadhi ya kazi feki za Wasanii zilizokamatwa.
Picha na www.burudan.blogspot.com
Kampuni
ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam inayosambaza kazi za
wasanii kwa kushirikiana na wasanii wamekamata kazi mbalimbali za
wasanii zinazorudifiwa kinyume na taratibu na kutofaidika kwa wasanii
wanaotoa kazi hizo.
Msemaji
wa Kampuni ya Steps Kambarage Ignatios amesema kuwa ukamataji huo si
wa zimamoto watahakikisha wanashirikiana na wasanii wenyewe kukamata
kazi zao maana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao zinatoka sana kumbe
zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa tu na kusubiri kazi
za wasanii ameiomba Serikali kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa
watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii.
Na
mmoja ya wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo iliyofanyika
makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii Mohamedi Nice
‘Mtunisi’ amesema watu hawa wana akili za ziada kwani katika kava ya
mbele wanaweka stika yetu halali na DVD ndio inakuwa imechakachuliwa
akiangua kilio na kusema wasanii wakifa wanakufa masikini kumbe ni watu
wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao bila kushiriki
chochote.
Baadhi
ya wasanii walioshiriki katika kamata kamata hiyo ni pamoja na Jacobo
Steven ‘JB’ Mzee Yusuph wa kundi la Taarabu la Jahazi Simoni Mwapagata
(Rado) Mussa Msuba wa iliyokuwa Segere Original Seles Mapunda ,Mohamed
Nice ‘Mtunisi’ na wengine wengi wasanii hawo wameungana pamoja kwa
ajili ya kutetea kazi zao ili zisirudufiwe kiolela na kuiomba serekali
kupitisha sheria kali kwa mtu anaekamatwa na kazi kama hizo.