Benki Ya KCB Tanzania Yatoa Msaada Hospitali Ya Wazazi Zanzibar


Katibu wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Bw.Omar Abdallah akipokea misaada ya vyandarua, mashuka pamoja na mashine ya kupumlia wagonjwa mahututi (Oxygen Conamtrator) vyenye thamani ya Milioni Tano kwa ajili ya Hospitali ya Wazazi ya Mwembeladu kutoka kwa Meneja wa Banki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Bw.Rajabu Ramia. Kulia ni Meneja wa Biashara wa Benki hiyo tawi la Zanzibar Bw.Abdallah Mshangama.

Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Bw.Rajabu Ramia, akimkabidhi Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar Bi.Zawadi Suleiman, Vyandarua na mashuka 50 vilivyotolewa na Benki ya KCB kama msaada kwa hospitali hiyo ya wazazi.
Afisa Uhusiano wa Benki ya KCB Tanzania Bi. Martha Edward akimpatia zawadi ya Tende Bi.Amina Ahamed alielazwa kwenye Hospitali ya Wazazi ya Mwembeladu Zanzibar mara baada ya wafanyakazi wa Benki ya KCB kufanya ziara katika hospitali hiyo mara baada ya kumaliza kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwenye hospitali hiyo.
Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Hospitali ya Wazazi ya Mwemberadu mjini Zanzibar, leo imepata msaada wa mashine ya kupumulia Wagonjwa mahututi, mashuka na vyandarua vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 kutoka Benki ya KBC Tanzania.

Akipokea msaada huo, kwa niaba ya Waziri wa Afya, Katibu wa Hospitali Kuu ya Zanzibar ya Mnazi Mmoja Bw. Omari Abdallah, amesema kuwa msaada huo utaiwezesha Hospitali hiyo kuweza kuwahudumia wagonjwa mbalimbali wakiwemo mama wajawazito na watoto wachanga wanaozaliwa kwenye Hospitali hiyo.


Hata hivyo Bw. Omar ametoa wito kwa makampuni mengine zikiwemo taasisi za fedha hapa nchini, kuendelea kutoa misaada ya hali na mali katika Hospitali na Zahanati ili ziweze kuboresha huduma kwa wagonjwa.


Awali akikabidhi Msaada huo, Meneja wa Benk ya KCB Tawi la Ston Town mjini Zanzibar Bw. Rajab Ramia, amesema benki yake imetoa misaada kama kwa Hospitali ya Mwananyamala na kusaidia madawati katika shule mbalimbali za Msingi za zanzibar na Dar es Salaam.


Wakati wa hafla hiyo, wafanyakazi wa Benki ya KCB wakiongozwa na Meneja Uhusiano wa Benki hiyo, Bw. Said Amour na Mneja wa Biashara Bw. Abdul Mshangama, walitoa zawadi mbalimbali kwa akina mama wajawazito na waliojifungua kwenye hospitali hiyo.