Aliyekuwa
Mbunge wa Arusha Mjini kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh
Godbless Lema akiunguruma kwenye uzindusi wa matawi katika Kata ya
Daraja Mbili Jijini Arusha juzi
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwasili kwenye Uwanja wa Kwa Mbombe katika kijiji cha Madizini, Kata ya Mtibwa mkoani Morogoro ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Opereshi Sangara
Aliyekuwa
Mbunge wa Arusha Mjini kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh
Godbless Lema amefungua matawi katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha
Katika
ziara hiyo, Lema aliambatana na Mbunge wa Arumeru Masariki Mh Joshua
Nassari(wa pili kulia) pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM kabla ya
kujiengua na kujiunga na Chadema mapema mwezi Aprili mwaka huu, Ndg
James Ole Millya, ambao nao kwa nyakati tofauti walipata fursa ya
kuzunumza.
Mbali
na suala la uzinduzi na upokeaji wanachama wapya, Lema alifanya
harambee ya kukusanya fedha kusaidia shughuli za chama hicho katika Kata
hiyo ambapo jumla ya Sh 219,500 zilichangwa na wananchi.
Akiondoka
eneo hilo, Lema alilazimika kuwatuliza mamia ya watu waliokuwa
wanafuatilia msafara wake ili kuepusha kutokea mwanya kwa watu wenye nia
mbaya kuleta vurugu na uharibifu wa mali. Baadae msafara wake
ulikatiza mitaa ya Stand Kuu ya mabasi makubwa na kisha kuelekea
bustani ya City Park huku njiani akishangiliwa sana na baadhi ya watu
wakinyoosha vidole kama ishara ya ushindi.
Wanachama wapya aliojiunga na chadema wakigombania kadi za chama hicho
Picha na Joseph Senga