Na Mwandishi Wetu.
Mwanamitindo
maarufu nchini Ally Rehmtullah ameandaa onyesho kubwa na la kipekee la
mitindo hapa nchini litakalofanyika tarehe 8 Mwezi ujao katika jiji la
Dar es Salaam na kuonyeshwa moja kwa moja katika mtandao wa www.ar.co.tz ambapo pia atazindua rasmi kazi zake mpya za mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanaume na wanawake.
Akizungumza
na vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Rehmtullah amesema
dhumuni la kuandaa onyesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha aina mpya
ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati zake za kuinua
kiwango cha kazi za mitindo ndani ya nchi.
Mesema
amepanga kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini ili
kazi za wanamtindo na wabunifu wa mavazi ziweze kupenya kwenye soko la
ndani na la Afrika mashariki na kati wakati tayari kuna soko la pamoja
katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Rehmtullah
amesema kwamba onyesho hilo litakuwa la kipekee kwa sababu mavazi na
onyesho litapambwa na rangi nyeupe, ubunifu wa hali ya juu pamoja na
muonekano mpya wa mavazi yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza
kuendana na utamaduni wa mwafrika.
Amesema
onyesho hilo litakalofanyika katika hoteli ya Serena litapambwa na
wasanii mbalimbali wa muziki na wacheza shoo kutoka sehemu mbalimbali.
Rehmtullah
amesema onyesho hilo itakuwa ni nafasi ya kipekee kwa yeye binafsi
kuonyesha muonekano mpya wa tasnia ya mitindo hapa nchini na nje ya nchi
ili kuonyesha ni kwa jinsi gani wanamitindo wa kitanzania wanavyoweza
kuonyesha kazi zao.
Ameongeza
kuwa tasnia ya mitindo kwa ujumla ina nafasi ya kipekee kwa wanamtindo
chipukizi kujitokeza na kuonyesha kazi zao kwa watu mbalimbali hasa
washika dau katika sekta hiyo.
Onyesho
hilo linategemewa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 400 wakiwemo viongozi
mbalimbali kama mawaziri, wabunge, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa
mashirika mbalimbali.
Onyesho hilo litakuwa ni la mialiko maalum na limepewa jina la Ally Rehmtullah 2013 collection.
Wadhamini
wa onyesho hilo ni Mercedez Benz, Belvedere Vodka, DULUX, RAHA, HUGO
DOMINGO,THE Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm Plant, Creative
Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia Properties, Dar es Salaam
Serena Hotel, Missie Popular Blog, MO BLOG,Quality Furniture na Mx Carter.