Stori za uhakika nilizozipata
muda mfupi uliopita ni kwamba mkali wa Hiphop kutoka A Town ambae alikua
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy
Dimpoz, Isack Waziri (Lord Eyes) hivi sasa yuko nje kwa dhamana.
Ametoka nje kwa dhamana toka ijumaa ya novemba 2 2012.
Oktoba 23 2012 Kamanda wa polisi
mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alikaririwaakisema “Watuhumiwa hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes tunawashikilia
kwa tuhuma zipatazo 30, yani matukio mbalimbali 30 pengine yanaweza
yakaongezeka ambayo yameripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali kama
vile Mlimani City, Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama Coco beach, kwenye
kumbi mbalimbali za starehe na pia kwenye maeneo ambayo kunakua na
harusi, sehemu ambazo kunakua na magari mengi watu hawa ndio huwa
wanaitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, tunawashikilia kwa makosa ya
wizi”