.
Polisi Kinondoni Dar es salaam imetangaza kukamata watu 38 kwenye oparesheni iliyoendeshwa kukamata watu waliofanya makosa mbalimbali ikiwemo ya kuuza miili na majambazi.Kamanda wa polisi Kinondoni Charles Kenyela amesema huo msako umewapa nafasi ya pia ya kukamata wasichana watano wakazi wa Mwananyamala wanaojihusisha na biashara ya kuuza miili yao Dar es salaam ambapo wakati wamekamatwa wamekutwa na dawa zilizosagwa pamoja na vidonge kwa ajili ya kuwalewesha watu wanaokutana tayari kwa kununua mapenzi na huweka hizo dawa kwa hao wateja kwenye vyakula na vinywaji alafu wakilewa wanawaibia na kukimbia.
Alichosema Kamanda ni kwamba hao wasichana wanashikiliwa na polisi ambapo dawa walizokutwa nazo zinaandaliwa kwa ajili ya kupelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali kwa vipimo kabla ya kuzipeleka Mahakamani kama ushahidi.....
kwenye huo msako pia kakamatwa jambazi mmoja anaitwa Haji Juma akiwa na bastola aina ya Bron na alikua anajiandaa kwenda kufanya uhalifu.