Njemba ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, amenusurika kifo kufuatia kuanguka ghafla na kupoteza fahamu kwa madai ya kuchanganywa na mauno ya Aunty Lulu
Mkasa huo ulijiri kwenye sherehe ndogo ya watu wa karibu baada ya msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kufunga ndoa na Gardner Dibibi, Kinondoni, Dar es Salaam wiki iliyopita.
Ilikuwa ni wakati wa ndugu, jamaa na marafiki wakipata msosi sanjari na vinywaji huku muziki ukipigwa nyumbani kwa familia ya bibi harusi, Kinondoni, ndipo Aunty Lulu alipoanza kukata mauno na kushangiliwa.
Wakati watu wakimpa dole Aunty Lulu, jamaa huyo alimtolea macho pima na kuanza kuchanganyikiwa na mauno hayo.
Polepole jamaa, mkono mmoja ukiwa umeshika sahani yenye msosi mwingine soda, aliganda kwa sekunde kadhaa kama vile haamini anachokiona.
Kufumba na kufumbua, njemba alikwenda chini ghafla na kupoteza fahamu.
Hali ya hewa ilichafuka kuanzia hapo, ikawa patashika nguo kuchanika.
Hata hivyo, wanaume majasiri waliokuwa eneo la tukio walimpepea jamaa huyo ambapo baadaye alizinduka.
Jamaa huyo baada ya kurejewa na fahamu alisikika akisema: Ukweli wowowo la huyu dada (Aunty Lulu) limenichanganya, nusu linitoe roho jamani.
Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema kilichomtokea jamaa huyo ni mfadhaiko.