CHELSEA YASAJILI KINDA LA BRAZIL




KLABU ya Chelsea imefanikiwa kumnyakuwa kiungo kinda wa kimataifa wa Brazil, Oscar kwa ada ya paundi milioni 25.

Pamoja na kutumia kiasi cha paundi milioni 42 kuwasajili Marko Marin na Eden Hazard, mmiliki wa klabu hiyo Roman Abromovic ameonekana kutaka kufanya mapinduzi ya ukweli baada ya kumsajili kiungo huyo aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Internacional. Kiungo huyo ambaye kwasasa ndiye anahesabika kuwa kiungo bora kupata kutokea nchini humo kwa miaka kadhaa pia alikuwa akiwindwa na aliyekuwa kocha wa zamani wa Chelsea Andres Villas-Boas ambaye kwasasa anainoa klabu ya Tottenham Hotspurs. Villas-Boas ambaye alitangaza kumtengea Oscar mwenye miaka 20 kiasi cha paundi milioni 11 wiki iliyopita lakini klabu hiyo ya Amerika Kusini ilikataa kiasi hicho na kuwaachia Chelsea ambao walitoa kiwango kikubwa zaidi. Nyota ya kiungo huyo ambaye majina yake kamili ni Oscar dos Santos Emboaba Junior iling’aa katika michuano ya Kombe la Dunia la vijana chini ya umri wa miaka 20 ambapo katika mchezo wa fainali alifunga mabao matatu pekee dhidi ya Ureno katika mchezo wa fainali na kuiwezesha timu yake kuibuka kidedea kwenye michuano hiyo.