OSCAR KUFANYIWA VIPIMO CHELSEA.
|
Oscar |
KIUNGO wa kimataifa wa
Brazil, Oscar amesema kuwa anatakiwa kufanyiwa vipimo vya afya na klabu
ya Chelsea ya Uingereza lakini atasubiria mpaka baada ya michuano ya
Olimpiki kumalizika ili kuamua hatma yake. Kiungo
huyo wa klabu ya Internacional ya Brazil mwenye miaka 20 kumekuwa na
tetesi kuwa klabu hiyo imemuuza kwa ada ya paundi milioni 25. Lakini
baada ya mchezo wa kirafiki ambao Brazil ilishinda mabao 2-0 dhidi ya
timu ya kombaini ya Uingereza, Oscar amesema kuwa bado hajakubali kutua
Chelsea ambayo ina maskani yake katika Uwanja wa Stamford Bridge. Oscar
amesema kuwa wachezaji wengi wa Brazil huwa wana ndoto nay eye kama
wenzake wengine naye ana ndoto za kucheza Ulaya na Ligi Kuu nchini
Uingereza lakini suala hilo itabidi nilitolee maamuzi baada ya michuano
ya olimpiki. Fainali ya michuano ya olimpiki inatarajiwa kuchezwa Jumamosi Agosti 11 mwaka huu.