Safari Za Mbeya Na Abrakadabra Za Wahubiri Wa Kikristo


Mhubiri wa madhehebu ya kipentekoste akihubiri kwenye basi la upendo la Iringa
Jana nikiwa safarini kuelekea Mbeya ,ghafla nasikia karibu kabisa na masikio yangu na kwa sauti kubwa,Halleluyah!,Bwana Yesu aisfiweeeee,na watu baadhi haraka wakajibu Ameen.yakaanza mahubiri mfululizo kwa takriban dakika 40 hivi.kwa kweli japo mimi ni mkristo lakini huaibishwa sana na wahubiri hawa.Kwani licha ya kusumbua watu,huhubiri kwa kelele na wakati mwingine wakidondosha mate hovyo,hawajali kama kati ya wasikilizaji wapo wanaoona kuwa mahubiri yao ni kero na labda ni matusi kwao.fikiria muislamu aliyelipa hela ili asafiri tu,ghafla anagundua kuwa kumbe ameingia kanisani,yawezekana ana watoto wake ambao asingependa wasikie upuuzi huu,analazimika kulishwa injili FEKI na heresy(kadiri ya uislamu) yesu si mungu,wala mwana wa mungu,hakuna utatu mtakatifu,wala yesu hakufa  msalabani.Acha huyo ni mwislamu,lakini kuna wakatoliki.mara utasikia kuna watu wanamwabudu maria,mara wanasali kwa masanamu,mara wanasema dhambi kwa wanadamu,nk wote hawa wasipompokea yesu wanaenda motoni.Hii ni ajabu na kwa kweli ni ujinga.kwa sababu licha ya wakristo hawa kupiga kelele,kukosa ustaarabu wa kawaida wa kuheshimu dini za wengine,wanafundisha uzushi na vitu vingi ambavyo ni kinyume na ukristo wenyewe.Mimi siku hizi siwavumilii tena.nimepaza sauti jana kueleza kukerwa kwangu,lakini kondakta hakujali,wala huyo mchungaji uchwara.nikaamua kuwasha sigara,ndipo kila mtu alipolalamika.nami nikawaeleza kwani sigara si ninavuta mimi,wengine inawahusu nini? wote wakanishambulia kuwa unawadhuru moshi wa sigara,nami nikawaambia ndivyo ninavyodhurika na moshi wa sigara ya mahubiri ya wachovu hawa.ubishi uliendelea baadaye bwana akaomba fedha kama sadaka ,nauli ya kurudia Dar.Ni uhuni tu na kuiba hela za watu,kwa sababu gari alipanda bure,na anarudi bure.Yaani wajanja wanatumia jina la yesu kuiba!!!
Haishangazi tanzania.Ilikuwa hivyo Loliondo na itaendelea,wizi kwa kutumia neno la mungu,kama anavyoita Mjengwa,hizi ni Abrakadabra,basi.na kwa kweli kama huu ndo ukristo,basi max alikuwa sawa alipouita bangi.Tafakari
Ludovick: 0753 927100