PORTO KUMUUZA MOUTINHO KWA PAUNDI MILIONI 31.
|
Moutinho. |
KLABU ya Porto
imethibitisha kuwa inaweza kumuuza mchezaji wake Joao Moutinho lakini
wameionya klabu ya Tottenham Hotspurs ambayo inamuwinda mchezaji huyo
kuwa watatakiwa kulipa kiasi cha paundi milioni 31.5 kama wanamuhitaji
kiungo huyo. Moutinho
amekuwa mchezji tegemeo kwa klabu na nchi yake ambapo meneja mpya wa
Spurs Andres Villas-Boas ambaye ameshawahi kumfundisha kiungo huyo
mwenye miaka 25 ni chaguo lake kubwa analohitaji. Kwasasa
kocha huyo bado hajafanya mawasiliano na Porto kuhusiana na mchezaji
huyo lakini wameonyesha nia ya kumhitaji mchezaji huyo na wako tayari
kuanza mazunguzo kuhusu kiwango hicho cha fedha kilichowekwa na porto. Meneja
wa Porto Votor Pereira amesema kuwa bado hajazungumza na Villas-Boas
kuhusiana na suala hilo lakini anaonekana kumtaka mchezaji huyo na wao
wanamhitaji lakini katika soka kama ikifikia wakati kama huu timu
inakuwa haina jinsi bali kumuuza na kuiletea faida klabu. Spurs
inamuhitaji Moutinho ili kuziba pengo la Luka Modric ambaye anaweza
kuondoka msimu huu baada ya vilabu vya Real Madrid na Paris Saint
Germain zikiitafuta saini yake kwa udi na uvumba.