Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL Kapteni Milton Lazaro
akizungumza na waandishi wa habari juu ya kushitisha kwa mkataba baina
ya shirika hilo na kampuni ya Aero Vista Dubai ambayo ilikodisha
shirika hilo ndege aina ya Boeing 737-500.
SHIRIKA
la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limesitisha mkataba wake na kampuni ya
Dubai ya Aero Vista kutokana na kuwa makubaliano yaliyofikiwa mapema
mwezi Mei hayakuleta maafanikio yaliyotarajiwa.
ATCL
ilikodi ndege aina ya Boeing 737 – 500 yenye uwezo wa kubeba abiria
108 mnamo mwezi wa tano ambayo imekuwa ikiitumia kufanya safari za Dar
es Salaam – Kilimanjaro- Mwanza na baadae kuzitumia katika safari
nyingine ya Dar es Salaam – Hahaya (Comoro) iliyozinduliwa mwezi
uliopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa ATCL Kapteni Milton Lazaro alisema kuwa shirika limefikia
uamuzi huo baada ya kugundua kuwa shirika halipati faida iliyokusudiwa
kabla ya kusaini mkataba huo.
Aidha,
Lazaro alisema kuwa shirika lipo katika mazungumzo na kampuni nyingine
ili kuafikiana katika kufanya biashara pamoja na kuongeza kwamba
mazungumzo hayo yanatarajia kukamilika katika wiki chache zijazo.
“Tumeamua
kusitisha mkataba tuliosaini na kampuni ya Aero –Vista kutokana na
ukweli kuwa mkataba huwo haujatuletea mafanikio tulieyeyekusudia. Kuna
uwezekano wa kujadiliana upya na tunaweza tukaingia nao katika mkataba
mpya baada ya mazungumzo kama wanaweza kuondoa baadhi ya vipengele
ambavyo si vizuri kwetu kama kampuni.
“Abiria
ambao tayari wameshakata tiketi katika kampuni yetu hawana sababu ya
kuwa na wasiwasi sababu tayari tumeshawakatia tiketi katika mashirika
mengine ambayo na safari zao zitaendelea kama walivyopanga,” alisema
Lazaro.
Aliongeza
kuwa shirika hilo la ndege la taifa litarudisha safari zake Dar –es
Salaam- Kilimanjaro-Mwanza baada ya kukamilika kwa matengenezo ya ndege
ya shirika hilo aina ya Dash 8Q-300 ambayo ipo katika karakana ya
shirika hilo kwa sasa.
Pia,
Kapteni Lazaro alisema kuwa safari ya Dar es Salaam – Kilimanjaro –
Mwanza ndiyo safari pekee itakayoathirika kutokana kusitishwa kwa
mkataba huwo na kuongeza kuwa shirika litaendelea na safari zake za Dar
es Salaam – Hahaya kama kawaida.
“Tunaomba
radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. Wateja wasifikirie kuwa hatupo
kabisa kwenye biashara. Tutaendelea na safari zetu za Dar es Salaam –
Hahaya (Comoros) kwa kipindi hiki. Ni safari za Dar es Salaam –
Kilimanjaro – Mwanza pekee ndizo zitakazodhurika katika kusitishwa kwa
mkataba huu,” alisema.