OFFICIAL: BARCELONA NA ARSENAL ZAKUBALINA ADA YA UHAMISHO WA ALEX SONG

Klabu ya FC Barcelona imetangaza jioni hii kwamba imefikia makubaliano juu ya ada ya uhamisho wa kiungo Mcameroon Alexander Song kutoka Arsenal.Song sasa atasafiri kwenda Barcelona ndani masaa 48 yajayo kwa ajili ya kufanya vipimo na kujadiliana huu ya maslahi binafsi kabla ya kusaini mkataba na Barcelona.

Uhamisho huu wa Song unakuja siku moja baada ya Robin Van Persie kukamilisha uhamisho wa kujiunga Manchester United akitokea Arsenal. Kuondoka kwa Song kunamaanisha Arsenal sasa itakuwa imeuza wachezaji wake muhimu waliocheza kwa kiwango kikubwa msimu uliopita na kuiwezesha kushika nafasi ya 3 kwenye ligi kuu ya England.


Alex Song anakuwa mchezaji wa nne wa Arsenal kujiunga ba Barcelona katika kipindi cha miaka 5 iliyopita, wa kwanza akiwa Thierry Henry, akafuatiwa na Alexander Hleb, Cesc Fabregas na sasa mcameroon huyo.